Michezo

Haji Manara afunguka kuzungumzia ishu ya kutimuliwa Simba

Kulikuwa na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Klabu ya Simba imeamua kumtoa kwenye nafasi ya Ofisa Habari, Haji Manara kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Taarifa hizo zilienea kwa kasi na kusambaa hasa kwenye magrouup ya mitandao ya kijamii, lakini hakukuwa na tamko rasmi kutoka Simba juu ya maamuzi hayo.

Manara amelizungumzia hilo kwa kueleza kuwa hakuna kitu kama hicho na kuwatolea ‘povu’ wale wanamchukia na kusambaza taarifa ambazo siyo za kweli.

Manara ameweka picha ya mtu aliyesambaza taarifa hizo kupitia Instagram kisha akaandika maelezo haya:

“Kuna mpumb** mmoja aliyejitambulisha kama Mwenyekiti wa Group la Yanga WhatsApp supporters makao makuu, anazusha mitandaoni kuwa nimeondoka Simba…hahahahaha sitakaa milele pale kama yeye na wapumb** wenzie watavyoondoka huko walipo, lakini kwa sasa mm ndiyo msemaji wa Big brand ya nch….. , unavyozidi kunichukia ndiyo unazidi kunisogeza…. Kwa mnaoniogopa wote niwaambie NA BAO.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents