Michezo

Haji Manara afunguka sakata la kuachishwa kazi Simba SC (+video)

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa anashangazwa na Watanzania kukomalia suala la yeye kuachishwa kazi ya usemaji wa klabu ile hali ni jambo la kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 20, 2019. Manara amesema kuwa yeye hatadumu milele kwenye nafasi hiyo ya kiti cha usemaji wa Simba, Hivyo ikitokea mtu mwingine akachaguliwa ataondoka na atampa sapoti.

Kwa upande mwingine, Manara amesema kuwa Simba ni klabu kubwa na hakuna mtu mkubwa ndani ya Simba SC, Ingawaje anaamini kuwa amefanya mambo makubwa kwa nafasi yake.

Klabu ya Simba mwezi Juni mwaka huu, Ilitangaza nafasi mpya ya msemaji wa klabu hiyo na nafasi nyingine ndani ya klabu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents