Tupo Nawe

Haji Manara amfundisha kazi kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amemtaka kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ajifunze kuongea vizuri mbele ya waandishi wa habari pindi timu yake inapofungwa.

Manara na Mwinyi Zahera

Haji Manara ametoa somo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo ameanza kwa kumsifia kocha wa Simba, Patrick Aussems kwa kitendo cha kuwapongeza wapinzani wake Kagera Sugar kwenye mchezo wa jana ambao Simba walifungwa goli 2-1 .

Tofauti ya kocha wa mpira na kocha wa Sunsumia au kibao kata!!. Unafungwa unawapongeza washindi na kukubali mapungufu yako, angekuwa yeye sasa!, “waamuzi wanatuonea, mimi nimefundisha Ulaya miaka arobaini”, ( ukigoogle ) huoni timu alizofundisha zaidi ya kufundisha kucheza ndombolo na mayenu ). “Ohh Simba inabebwa, leo sikushinda kisa Ajibu na Fei Toto hawakuvaa boksa na hawajala toka juzi!!. Ila akishinda sasa, najua kupiga gitaa kuliko Diblo, na ile fasi ya putuluu imekuja na ndege na ndio maana sisi Wakongo tunapendwa na wadada wa bongo. Kocha mzuri huzungumzia vitu ‘technical’ na sio riwaya za wanaotumia mkorogo wa buku buku!!!“. ameeleza Manara.

Tayari Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameshamuomba Manara aache kumzungumzia yeye wala klabu yake ya Yanga na aendelee kufanya kazi zake ndani ya klabu ya Simba.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW