Michezo

Haji Manara amtaja mchawi anayeipeleka shimoni Manchester United

Kufuatia matokeo hafifu ya Klabu ya Manchester United kwa mechi tatu mfululizo kumepelekea Msemaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuweka wazi sababu za matokeo hayo mabovu.

Haji Manara amesema mtu pekee anayesababisha matokeo mabovu ni Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Jose Mourinho kutokana na mfumo wake mbaya wa kupaki basi.

Manara amedai kuwa klabu yenye wachezaji wazuri kama Manchester United haipaswi kucheza mfumo wa kujilinda kama itahitaji matokeo mazuri.

Anayetuingiza huko (Shimoni) ni huyu ‘kijuso’ Mourinho..hivi una Mikhtaryan,Martial,Pogba,Mata na wengine..kisha unatumia mfumo wa kupaki basi? sina raha kuona team yangu ikicheza vile, I hate Jose, DSTV sijalipia mwezi huu coz of Jose..kwendraaaaaa Mourinho.“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye michezo mitatu, Manchester United imepoteza mchezo mmoja wa Kombe la EFL na kutoa sare michezo miwili ya Ligi kitu ambacho kimeanza kuleta maswali mengi kwa mashabiki wa klabu hiyo wengi wakichukizwa na mfumo wa Kupaki basi unaotumiwa na Mourinho.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents