Michezo

Haji Manara amvulia kofia Ibrahim Ajib

Msemaji mkuu wa Klabu ya Simba, Haji Manara amemwagia sifa aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajib ambaye kwa sasa anachezea Yanga kwa kudai ameondoka ndani ya timu hiyo bila ya maneno ya dharau.

Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara.

Manara amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema afanye kazi yake vizuri kwani muda wowote ule anaruhusiwa kurudi Msimbazi .

Najua nini unamiss dogo ila kafanye kazi hapa ni home anytime!! umeondoka bila maneno ya hovyo umetuheshimu na sisi tutakupa heshima yako nakuhakikishia hutasumbuliwa na fan yoyote wa Simba ustaarab upo nyonyoni mwetu”,ameandika Haji Manara.

 Ajib kwa sasa anachezea klabu ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC ambapo amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili katika dirisha la usajili wa msimu mpya wa Ligi 2017/2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents