Michezo

Haji Manara apewa onyo kali na kamati ya TFF

Mbwembwe za Haji Manara zimeanza kumponza. Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, imempa onyo kali Mkuu huyo wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba kwa kosa la kuingia uwanjani.

Kiongozi huyo alifanya kosa hilo Jumapili iliyopita wakati wa mechi ya watani wa jadi ambapo Simba aliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Katika barua hiyo iliyotolewa imemtahadharisha kiongozi huyo kwa kuendelea kufanya matukio mengine kama hayo na endapo ataendelea kamati hiyo itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi yake. Soma barua hiyo hapa chini:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents