Michezo

Haji Manara atema cheche baada ya kutwaa Ngao ya Jamii (Video)

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ushindi wao walioupata dhidi ya Yanga SC katika mtanange wa Ngao ya Jamii unatokana na ubora wa kikosi walicho nacho msimu.


Manara ameyasema hayo alipozungumza na Bongo5 wakati akishangilia ubingwa huo walio upata kwanjia ya mikwajju ya penati 5-4.

Manara amesema, “Timu bora siku zote inashinda haijalishi ni katika mazingira gani lazima ipate ushindi na mipango yetu ilikuwa ni kupata magoli matano kwa mazingira yoyote yale iwe ni penati ama ndani ya dakika 90 ilikuwa lazima yapatikane hivyo tunashukuru ni mwanzo mzuri wa ligi.”

Ameongeza, “Mara ya mwisho niliwaambia Yanga kama waamuzi wakichezesha kwa haki hawatatufunga kokote mechi zote walizoshinda walikuwa wakibebwa kwa hiyo nawaomba shirikisho lampira wa miguu Tanzania (TFF) waendelee kupanga waamuzi bora hata huyu waleo alikuwa na mapungufu lakini ya kwake ni ya kibinadamu kila mtu ameyaona kwa pande zote mbili.”

“Kesho kikosi chetu kitapumzika ila tutaingia kambini jioni kwaajili ya mechi yetu ya Jumamozi dhidi ya Ruvu Shooting tunawashukuru sana wachezaji wetu wamefanya kazi kubwa sana lakini pia wengi bado wapya hivyo mwalimu ataendelea kuiboresha zaidi,” amesema Haji Manara.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents