Michezo

Manara atoa ufafanuzi juu ya kumshabulia Shaffih ‘Sina Ungomvi nae nalinda Brand ya Simba’

Manara atoa ufafanuzi juu ya kumshabulia Shaffih 'Sina Ungomvi nae nalinda Brand ya Simba'

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametoa ufafanuzi juu ya kile kilichopelekea kumshambulia mwandishi wa habari wa Clouds Fm Shaffih Dauda kuhusu kile alichokipost jana na vingine anavyoviandika vinavyoihusu klabu ya Simba.

Mnara amesema:- ” Morning !!
Nimeamua kuufunga mjadala kwa maneno haya ,
Guys mm ni mwajiriwa wa Simba na moja ya jukumu langu ni kuitetea na kuihami klabu yangu kwa kila hali! Watu wanadhani majibu yangu ya jana kwa @shaffih ni kwa kuwa kapost hzo tetesi tu!
Sio Siri shaffih Mara kadhaa amekuwa akiandika vitu vibaya kuhusu Simba,na always nalaumiwa mm kwa kumuachia na wengi husema coz naonekana nae somewhere tukichill ndio maana simjibu!!
Wengi mnakumbuka uzushi aliouleta wa Simba kufungwa 5 huku South,mnaikumbuka vema issue ya Singano na kesi!!bado aliwahi kusema vibaya juu ya transformation yetu na mambo kadha wa kadha!!
Simba ni taasisi na inahitaji iheshimiwe kama cc tunavyoheshimu mahali anapofanyia kazi yy !haiwezekani kila siku ni yy tu against us na tuendelee kumkalia kimya!
Simchukii na yy anajua but pia siwezi kuona klabu yangu inasakamwa na mtu mmoja daily nikawa nipo kimya!
Issue ya Haruna hata kama ni tetesi haiwezi kuwa ktk engo ile zaidi ya mwendelezo wake!! Na kila mtu ndani ya Clouds anajua malalamiko ya Simba juu yake! Mabosi wakubwa wote wa clouds washalalamikiwa na uongozi wetu juu ya mwenendo wake,na yy anazidi tu kila mara!! Narudia hadi mm niondoke Simba au nife ndio mtu aidhalilishe hii klabu na kwake yy hili litakuwa onyo la mwisho,uzushi na uongo wowote ni kwenda baraza la habari tu!
Watu mmesahau majuzi tu walizusha tumefungwa saba na madereva taxi?
Noooo nasema Noooo!
Imetosha sasa!!
Image ya club yangu italindwa kwa jasho jingi sana wakati huu tukiwa ktk Simba mpya.. Mjadala huu nimeufunga na sasa tuelekeze nguvu Lesotho.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents