HabariUncategorized

Haji Manara, Jacqueline Wolper walizwa na mauaji ya watoto mkoani Njombe

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara na Muigizaji wa filamu, Jacqueline Wolper wameonesha kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya watoto yanayotokea mkoani Njombe.

Manara na Wolper

Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Tupaze sauti zetu wote kukemea dhulma hii!! Watoto wanayo haki ya kuishi,haki ya kusoma na wanayo haki ya kucheza na kufurahi! Why wauawawe ? Ndugu zangu hili ni jukumu letu sote kuwalinda watoto wetu,kulilinda Taifa letu la baadae,tusikubali udhalimu huu,na tuseme NO!! Inaumiza sana kuona yupo Mtanzania anafanya ukatili huu kisa ni imani potofu za kishirikina!!
Khofu ya Mungu ipo wapi? Ohhh Watoto wetu nn kosa lao? Au kuzaliwa watanzania? ! Mwenyezi Mungu kwako tunakukabidhi wauaji hawa waliolaanika
.”

Wolper yeye ameandika “Jesus eti Nini kina endelea sijaelewa 😳 Hii ni Tanzania Then why 🙆‍♀️How🤔 Coment This kwa wanaojua Na poleni Wote 🙏”.

Kwa wiki mbili sasa kumekuwa na taarifa za mauaji ya watoto mkoani Njombe, ambapo serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa taarifa bungeni kuwa mauaji hayo yanahusiana na mambo ya kishirikina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents