Habari

Video: Hakuna aliyethibitishwa kuwa na Ebola nchini – Waziri Ummy

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema hakuna mtu aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania huku ikiwataka Watanzania kuwa na hofu juu ya ugonjwa huo.

Akizungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa hatua mbalimbali zinachukuliwa kuhusu kujikinga na ugonjwa huo usiingie nchini.

“Hakuna mtu aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania hivyo watanzania msiwe na hofu ila tuchukue tahadhari na kupata elimu zaidi ili kujikinga na ugonjwa huu” alisisitiza Waziri Ummy.


Waandishi wa habari wakimsikiliza, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Aidha Ummy alisema kuwa serikali imeongeza mashine nne za kupimia virusi vya ugonjwa wa Ebola katika mipaka ya Holoholo,Mutukula,Rusumo na Silali ili kudhibiti na kutambua hali ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa wasafiri wa ndani na nje ya Tanzania.

“Moja ya hatua tuliyochukua kama Wizara ya Afya ni kuweka mfumo wa kufuatilia magonjwa (Intergreted Disease available system) na kujua  taarifa za wasafiri katika mipaka yote kwa  wanaotoka nchini Congo kuingia Tanzania ili kujua wanapotoka mpaka wanapofikia hakuna maambukizi ya ebola ,” alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa mbali na hatua hizo Serikali imegawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Ebola ikiwemo gauni la kujikinga,mawani,mabuti pamoja na vidonge vya Chroline katika mipaka yote ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa watumishi wanaofanya kazi mipakani.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa kuweka mabango yanayohusu ebola katika mipaka yote na vituo vya kusafiria ikiwemo viwanja vya Ndege,Bandari na vituo vya mipakani na kupitia njia ya simu kwa kupiga namba 117 kwa mitandao yote.

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents