Burudani

Hakuna anayeniweza kwa chochote – Dogo Janja

By  | 

Dogo Janja ni msanii aliyechipukia kimuziki miaka ya nyuma na kujitengenezea jina na nafasi kwenye tasnia kutokana na ubora wa muziki wake na pia swagga zake za mavazi. Juzi kati, dogo amefanya interiview na Times FM na kufunguka mengi ikiwemo Madee na nafasi yake kwenye maisha yake kimuziki na kuhusu hakuna anayemuweza kwa chochote.

Ukiachilia mbali Madee kuwa baba wa kimuziki kwa Dogo Janja lakini pia amechukuwa nafasi kubwa katika maisha ya Rapper huyo.

Akiongea katika kipindi cha Twenzetu cha Times FM, Janja amemshukuru sana Madee kwa kuendelea kufanya naye kazi huku akihisi kuwa kama isingewezekana kwa Madee kumpokea na kufanya naye kazi asingeweza kufanya muziki kabisa.

Hitmaker huyo wa Kidebe, amefunguka kuhusu kauli ya Young Dee aliyoitoa Jumamosi iliyopita katika kipindi cha The Playlist kuhusu kumzungumzia vibaya yeye pamoja na Young Killer.

“Sidhani kama huu ni muda wa kumzungumzia Young Dee. Muziki ninaofanya mimi ni mkubwa, Young Dee sio level yangu kabisa, natakiwa kuzungumzia vitu vikubwa. Hakuna ambaye ananiweza kwa chochote, narudia tena hakuna ambaye ananiweza kwa chochote ,” ameongeza Janja.

Kwa sasa Dogo Janja ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Ukivaaje Unavaaje?’.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments