Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hairuhusiwi kufanya adhabu ya mtu mwingine, kosa linabaki kuwa la mkosaji – Waziri Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya adhabu ya mtu mwingine na kosa linabaki kuwa la mkosaji.

Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Devotha Minja,ameihoji serikali kuwa, “Hivi karibuni kumezuka na tabia mbaya kwa Jeshi la Polisi wanapoenda kumkamata mtuhumiwa wakimkosa wanamkamata mtu mbadala akiwa Mke au watoto, Naomba kufahamu Jeshi la Polisi linatoa wapi mamlaka haya ambapo wanashindwa kutumia mbinu zao za Kiintelijensia kukamata mtuhumiwa badala yake wanarahisisha kuwakamata mama au mtoto na kuwatesa?

“Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria na niseme pia hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya adhabu kwa mbadala , kosa linabaki kuwa la mkosaji kwahiyo nieleke tu popote pale ambapo mtu amefanya kosa atafutwe yule yule aliyekosa na kama wengine wanaweza wakasaidia basi wasaidie kwa namna ya kuelezea jinsi wanavyoweza kufahamu sio kuchukua adhabu ya mtu mwigine aliyekosa,” amesema Mwigulu leo, Juni 13, 2018 Bungeni jijini Dodoma.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW