Hakuna mshindi wa tuzo za Mo Ibrahim 2012

Kwa mwaka wa tatu mfululizo, kamati ya tuzo za uongozi bora barani Afrika za taasisi ya Mo Ibrahim imetangaza kuwa hakuna mshindi wa mwaka huu.

Tuzo hizo ambazo huambatana na kitita cha dola milioni 5 zilizoanzishwa na mjasiriamali mzaliwa wa Sudan Mo Ibrahim hutakiwa kutolewa kila mwaka kwa rais wa Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia ambaye ataonesha uongozi bora na ambaye amestaafu mwenyewe.

Lakini kwa miaka sita sasa hakuna mshindi aliyepatikana.

“The Prize Committee of the Mo Ibrahim Foundation announces there is no winner of the 2012 Mo Ibrahim Prize #MIFPrize,” wametweet waandaji wa tuzo hizo.

Miongoni mwa marais wastaafu waliowahi kushinda ni pamoja na rais wa Botswana Festus Mogae, Joaquim Chissano wa Msumbiji na Pedro Verona Pires wa Cape Verde.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents