Hakuna Mtanzania aliyeingia kwenye fainali ya tuzo za ‘CNN Multichoice African Journalist Of The Year 2013’
Aibu yetu au ya nani? Hii ni habari mbaya kwa sekta ya habari Tanzania kwamba hakuna mwandishi/mtangazaji wa Tanzania aliyechaguliwa kuingia kwenye fainali ya tuzo za ‘CNN Multichoice African Journalist Of The Year 2013’
Hata hivyo Kenya imebahatika kuwa na waandishi sita huku wengine wakitokea Afrika Kusini, Nigeria, Uganda na kwingineko.
Akitangaza majina hayo, mwenyekiti wa panel ya majaji Feria Haffajee amesema walipokea majina kutokana nchini 42 barani zikiwemo nchi zinazozungumza Kifaransa na Kireno. Washindi watatangazwa kwenye tuzo hizo zitakazotolewa jijini Cape Town, Afrika Kusini Jumamosi ya October 12 ambapo mtangazaji wa CNN, Isha Sesay atakuwa host.
Haya ndio majina 27 ya waandishi walioingia fainali kutoka nchini 11:
Gifty Andoh Appiah, Joy News TV, Ghana
Rebekah Awuah, GBC 24, Ghana
Domingos Bento, Seminário Novo Jornal, Angola
Thomas Otieno Bwire, Pamoja FM, Kibera, Kenya
Axcel Micael Chenney, Le Défi Média Group, Mauritius
Florence Dallu, Freelance for Koch FM, Kenya
Nicola de Chaud, Freelance for Carte Blanche, South Africa
Adrian de Kock, The Star, South Africa
Ibrahima-Benjamin Diagne, Radio Futurs Médias (RFM), Senegal
Msindisi Fengu & Yandisa Monakali, Daily Dispatch, South Africa
Selma Inocência, Rede de Comunicação Miramar, Mozambique
Geoff Iyatse, The Guardian, Nigeria
Thanduxolo Jika & Media 24 Investigations Team, Media 24, South Africa
Judy Jeptum Kosgei & Mauritius Oduor, Citizen TV, Kenya
Lucas Ledwaba, City Press, South Africa
Lázaro Mabunda, O País, Mozambique
Carol Natukunda, New Vision, Uganda
Amon Ngabo, Uganda Broadcasting Corporation, Uganda
Tolu Ogunlesi, Freelance for Ventures Africa, Nigeria
Oluwatoyosi Ogunseye, Sunday Punch, Nigeria
Brenda Okoth, The Star, Kenya
Nassima Oulebsir, El Watan, Algeria
Passant Rabie, Egypt Today, Egypt
Roseline Wangui & Wambui Kurema, NTV, Kenya
Soma zaidi kuhusu kutangwazwa kwa majina hayo kwenye website ya CNN HAPA.