Habari

Hakuna mwenye mimba atakaerudi shuleni – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema wakati wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.

Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani.Ambapo leo ndio ilikuwa siku ya tatu.

“Mtu amezaa iwe kwa makusudi iwe kwa raha zake akienda shuleni si atawafundisha wenzie? Yaani tusomeshe wazazi.Katika utawala wangu hakuna aliyezaa atakayerudi shuleni.” Hawa watu watazaaa mno, sababu huo mchezo ni mzuri, katika kipindi changu kama Rais ukipata mimba kwaheri.Mwisho utakuta darasa la kwanza wote wana watoto wanawahi kunyonyesha,kwasababu mchezo huu ni mzuri.Hizo NGO’s zitalipeleka taifa pabaya na hao sijui na wenyewe wakafungue shule za wazazi, siyo zilazimishe serikali kusomesha wazazi,”alisema Rais Magufuli.

“Ndani ya utawala kama Rais hakuna mwenye mimba atakae rudi shuleni, hakuna mwenye mtoto katika darasa la kwanza mpaka sekondari atakaerudi shuleni amechagua hayo maisha ya mtoto akalee mtoto lakini hata kama amepata mimba kwa bahati mbaya yapo mambo mengi ya kufanya ambayo yana ruhusu watu waliojifungua.”

Aidha Rais Magufuli alisema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) anaweza akajifunza kushona cherehani anaweza akaenda kukopa akaanza kilimo cha kisasa anaweza akafanya shughuli nyingine.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents