Michezo

Hakuna timu itakayotoka na pointi Azam Complex – Cioaba

Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Aristica Cioaba, ameweka wazi kuwa anakiamini kikosi chake kuelekea mchezo wa Jumatatu ijayo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Mtibwa Sugar na kamwe hayupo tayari kuruhusu timu pinzani kutoka na pointi tatu katika Uwanja wake wa nyumbani.

Cioaba ameuambia mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa hawezi kuruhusu timu pinzani iharibu kazi yao katika viunga vya nyumbani huku akikiri kuwa haitakuwa  kazi rahisi kuibuka na ushindi.

“Kila mechi tunayocheza hapa Azam inakuwa ngumu timu zote pinzani zinataka kucheza vizuri dhidi ya Azam FC kila mmoja anahamasika, lakini wachezaji wanafahamu hii hali, nimewaona wamekuwa waangalifu wanapoingia kwenye mechi na kushinda mechi.”Amesema Cioaba

Aristica Cioaba  ameongeza “Naiamini timu yangu kuwa mechi ijayo hapa Chamazi itakusanya pointi zote tatu, kwani sitaki kutoa nafasi hapa kwenye uwanja wangu kwa timu pinzani kuharibu kazi yetu. Morali ipo juu kwa wachezaji, wamerudi wakitoka kwenye mchezo uliopita Njombe na wameshinda, wachezaji wanafuraha, siku hizi mbili za mazoezi wametulia.”

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 22 sawa na Simba SC iliyokileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Mtibwa Sugar ikijikusanyia pointi 17 katika nafasi ya tano sawa na Singida United iliyojuu yake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents