Burudani

Hakuna wimbo bora wa hip hop uliotoka baada ya ngoma yangu Wana Ndoto – Kala Jeremiah

Kala Jeremiah anaamini kuwa Wana Ndoto ni wimbo bora zaidi wa hip hop kutoka katika kipindi cha mwaka 2016/17.

Amedai kuwa tangu utoke, hajaona wimbo wenye kufikia ukali wake, hali inayomfanya asiachie ngoma mpya kwa sasa.

“Sijaona wimbo mkali wa kuushinda Wana Ndoto kwa ngoma zote za hip hop zilizotoka,” amesema rapper huyo.

“Hivyo nikisema nitoe wimbo mpya ni sawa na Mugabe ampindue Mugabe sasa ndio nini? Mimi ni mwana hip hop kweli kweli na najua hip hop, ndio maana nakuambia 2016/17 ngoma zote za hip hop zilizotoka ni unga unga, cheche, miyeyusho,” amejigamba Kala.

Imeandikwa na Nelson Munema (Mtangazaji, VMix – Channel Ten)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents