Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hali ya Marcus Rashford bado tata

Hali ya kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United, Marcus Rashford bado tata baada ya kushindwa kushiriki mazoezi wakati taifa lake likijiandaa dhidi ya Tunisia mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Dunia utakao pigwa siku ya Jumatau.

Hali hiyo inakuja mara baada ya Rashford kuumia kifundo cha mguu wakati timu yake ya Uingereza ilivyokuwa kwenye kempu ya mazoezi huku ikielezwa kuwa hakuumia mahala pakubwa.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Rashford amewashukuru watu mbalimbali ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa kumtakia heri.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, amelazimika kufanya mazoezi peke yake ‘Gym’ wakati kikosi cha timu yake ya taifa ya Uingereza kilivyokuwa Hoteli.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW