Burudani

RIPOTI: Hali ya Rick Ross yazidi kuimarika baada ya kupoteza fahamu

Big Boss wa Maybach Music Group , Rick Ross alikimbizwa hospitalini mapema hapo jana baada kupata tatizo la kushindwa kupumua na kupoteza fahamu.

Mtu wa karibu na raper huyo aliweza kupiga simu ili kwenda kumchukua mkali huyo na kumpeleka hospitali kwa ajili ya kupata matibabu
Kwa muibu wa mtandao wa TMZ, umeeleza kuwa Rick kwa sasa amewekewa machine za kupumulia za Oxygen ili kumsaidia aweze kukaa sawa na kupambana na tatizo hilo la nimonia.

Rapper Fat Trel ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa julisha mashabiki wao kuwa mkali huyo anaendelea vizuri kwa sasa.licha ya kuwa bado yupo chini ya uangalizi.

“JUS TALKED 2 MY BIG HOMIE… HE GOOD… HE IN DA HOSPITAL BUT HE IS NOT ON “LIFE SUPPORT” … HE GOOD,”

Hii sio mara ya kwanza kuripotiwa kwa taarifa za Rick Ross kupoteza fahamu na hata kusadikika kuwa na kifafa. Oktoba, 2011 Rozay alianguka kwa kifafa mara mbili, huku akidai ni kufanya kazi sana na kukosa usingizi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents