Michezo

Hali ya Shiza Ramadhan Kichuya yaimarika

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na Klabu ya soka ya Simba, Shiza Ramadhan Kichuya anaendelea vizuri baada ya kupata maumivu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC uliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa za mtan dao wa kijamii wa Instagram wa klabu ya Simba umeeleza kuwa mchezaji huyo anaemdelea vizuri.

“Kichuya anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa Daktari wa Timu Yassin Gembe,” imeeleza klabu hiyo kupitia mtandao wake wa Instagram.
Klabu hiyo imeongeza kuwa “Kichuya alipata maumivu kwenye kifundo cha mguu Kwenye mechi dhidi ya Mbao FC”.

Katika mchezo huo namba 25 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya mwenyeji wa mtanange huo klabu ya Mbao FC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents