Habari

Halima Mdee aianza wiki uraiani

Hatimaye Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee ameachiwa wa dhamana baada ya kusota rumande kwa zaidi ya saa 48.

Katika kesi yake iliyoanza kusikilizwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni kumi, pamoja na wadhamini wawili kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha fedha.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena August 7 ya mwaka huu mahakamani hapo.

Halima Mdee wiki iliyopita alitiwa mbaroni jeshi la polisi kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa tuhuma za kutoa lugha Chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents