Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Radio 1Xtra ya UK

Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha.

Baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya nchini Uingereza.

‘Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ .

Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW