Tupo Nawe

Halmashauri yavunja mkataba wa Tsh Bilioni 7.2  ujenzi wa stendi ya Mkoa

Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu imevunja mkataba wa shilingi bilioni 7.2 wa ujenzi wa stendi ya Mkoa wa Simiyu na mkandarasi ambae ni makampuni mawili yaliyongana ya Kings builders LTD na Halem construction ltd waliokua wakijenga stendi ya Mkoa wa Simiyu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Merckzedeck Humbe amesema wameamua kuvunja mkataba huo kutokana na kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo ambae amekua akijenga stendi hiyo kwa kusua sua pamoja na kupewa onyo mara kwa mara.

Katika kuahikisha ujenzi wa stendi hiyo unaogharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 7.2 unakamilika ndani ya muda, Mkuu wa Wilaya ametoa siku mbili kwa mkurugenzi kumpata mkandarasi mwingine atakaefanya kazi usiku na nchana na kuukamilisha Ujenzi huo ndani ya mwezi mmoja na nusu – hadi November 30 Mwaka huu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Azam Media Mkandarasi huyo alitakiwa kuukamilisha ujenzi huo may, 20 2019 alishindwa kufanya hivyo kwa madai ya kutopata msamaha wa Kodi (VAT) ambapo serikali ilimtaka kuendelea na ujenzi wakati suala hilo likishughulikiwa na kumuongeza muda hadi Sept 2, mwaka huu, muda ambao pia alishindwa kutekeleza na kuomba kuongezwa muda tena hadi Feb 1, 2020.

Mkandarasi huyo alikwishalipwa kiasi cha zaidi ya bilioni 5.1 na mpaka Sasa ujenzi wa barabara ya stendi umefikia asilimia 95, ujenzi wa eneo la maegesho asilimia 95 na jengo la abiria asilimia 80.

Kwa mujibu wa makubaliano ya serikali na Benki ya Dunia waliotoa fedha hizo, mradi unatakiwa kukamilika tarehe 31 December 2019 na endapo mradi hautokamilika fedha zitarudishwa, hali ambayo Mkurugenzi amesema kama halmashauri hawako tayari kuona fedha zinarudishwa kwa kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW