Burudani ya Michezo Live

Hamis wa BSS arudishwa kwenye mashindano hayo, Master J ashangaa kurudishwa kwake

Baada ya kelele za mashabiki wa BSS juu ya muimbaji Hamis kuondolewa kwenye mashindano hayo, hatimaye muimbaji huyo usiku wa jana amerudishwa na Chief Judge, Madam Ritta.

View this post on Instagram

BURUDANI: Hamis wa BSS arudishwa kwenye mashindano hayo, Master J ashangaa muimbaji huyo kurudishwa kwenye mashindano. Baada ya kelele za mashabiki wa BSS juu ya muimbaji Hamis kuondolewa kwenye mashindano hayo, hatimaye muimbaji huyo usiku wa jana amerudishwa na Chief Judge, Madam Ritta Madam amesema muimbaji huyo ameingia top 20 baada ya mshiriki mmoja kujiondoa kwenye mashindano kutokana na shughuli zake binafsi. Master J ambaye ni mmoja kati ya majaji wa mashindano hayo alionesha kutofurahishwa na kitendo hicho. Naye Hamis baada ya kutajwa kwamba amerudi, alipanda stejini hapo na kuyashukuru mashindano hayo. Awali Madam Ritta alidai mshiriki huyo alishindwa kuendelea na mashindano hayo baada ya ratiba ya BSS kuingilina na ratiba ya shule ya kijana huyo hali iliyoadhiri maendeleo yake katika mashindano hayo. Written and edited by @yasiningitu

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Madam amesema muimbaji huyo ameingia top 20 baada ya mshiriki mmoja kujiondoa kwenye mashindano kutokana na shughuli zake binafsi.

Master J ambaye ni mmoja kati ya majaji wa mashindano hayo alionesha kutofurahishwa na kitendo hicho.

Naye Hamis baada ya kutajwa kwamba amerudi, alipanda stejini hapo na kuyashukuru mashindano hayo.

Awali Madam Ritta alidai mshiriki huyo alishindwa kuendelea na mashindano hayo baada ya ratiba ya BSS kuingilina na ratiba ya shule ya kijana huyo hali iliyoadhiri maendeleo yake katika mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW