Habari

Hamisi Kigwangalla aamua kumsamehe Mo Dewji, alinidhalilisha ila nimesamehe

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameandika ujumbe huu:-

“Nilikutanishwa na Mohammed Dewji na baba yake, Mzee GMD. Kipindi hicho tuki-supply MeTL marobota ya pamba kutoka kiwandani kwetu. Alikuwa Mbunge wa Singida Mjini na mimi nikiwa nafanyia kazi ndoto zangu za kuingia bungeni. Kuanzia hapo tulikutana mara nyingi, zaidi kibiashara. Mwaka 2010 sote tulibahatika kuingia bungeni. Tulijenga urafiki na kushirikiana mambo mengi. Tuliunganishwa na mambo mengi; upenzi wa @simbasctanzania, siasa, na ujasiriamali. Kwa mahusiano/historia hii haikuwa tabu kumwomba mkopo wa pikipiki, tena wa mwezi mmoja tu. Mimi kama mkulima/mfanyabiashara ya mazao, ninakuwa na ‘stock’ ambayo huuza bei zikichangamka. Na yeye si mgeni kwenye hili. Ndiyo biashara. Kwa kuwa yeye ni jamaa yangu, na ana stock ya pikipiki, kuniazima haliwezi kuwa jambo zito saaana, kama naweza kuweka dhamana. Wapiganaji mjini tunafanya sana hii. Kwa wale maskini wenzangu, kukopa ni upiganaji unaosaidia kufanikisha jambo na wala siyo jambo la aibu, kimsingi ni harakati ya kupambana na umaskini. Kama hujawahi kukopa, basi haujapigana ipasavyo, ongeza bidii! Inawezekana nilihoji maswali magumu juu ya mustakabali wa ‘transaction’ ya Simba. Inawezekana nilimkera jamaa yangu. Lakini hakupaswa kwanza kutoa ‘Siri’ za kibiashara hadharani, jambo lililolenga kunidhalilisha, pili kuitumia hii situation kutoa majibu ya maswali ya msingi niliyouliza. Kunidhalilisha na kunichafua, nilijua tu ingekuwa ni ‘quick fix’ ya muda tu, isingesaidia lolote, sababu nilijua kuna mambo mengi ya msingi hayakuwa sawa kwenye ‘transaction’ yote. Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa Mohammed siyo wa kudharau kwenye hili, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba as a brand, siyo bure tu. Thamani ya Simba siyo majengo, ni brand yenye umri wa zaidi ya miaka 80. Tanzania ni lazima uwe Simba ama wale wengine…hata kama unamiliki timu yako. Siyo kitu kidogo. Simba ina maslahi ya umma. Ninaweza kusema mengi lakini siyo lengo langu. Nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana. Yaishe. Tusonge mbele. Naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza. Mimi nimesamehe. Maisha yaendelee. #HK #NguvuMoja 💪🏾”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents