Burudani

Hanscana amjibu Nisher ‘You talk about numbers, we talk about success’

Muongozaji wa video aliyekuja kwa kasi nchini, Hanscana hatimaye ameijibu kauli ya Nisher aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita kupitia mahojiano na Bongo5 kuwa Hanscana na Khalfan si tishio kwake na kwamba hawezi kushindana nao kwakuwa anawazidi kila kitu.

page

Hanscana ambaye ameongoza video ya wimbo wa Vanessa Mdee na Barnaba ‘Siri’ ametumia Instagram kupost ujumbe ambao kwa wale ambao hawakuona interview hiyo ya Nisher wanaweza wasielewe amemaanisha nini.

“U talk about number We talk about success….. JE UNAVIDEO GANI VEVO? IMEJIPOST TU,” ameandika Hanscana.

Tukumbushe kidogo, akiongea nasi mwezi uliopita, Nisher ambaye hivi karibuni aliongoza video ya XO ya Joh Makini na 13 ya Young Killer, alidai kuwa hatua ambayo Hanscana na swahiba wake Khalfan wapo, ndio ile aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita wakati akitafuta nafasi kama muongozaji wa video.

Khalfan aliwahi kuwa msaidizi wa Nisher na alipoondoka wawili hao waliingia kwenye vita vya maneno kwenye mitandao ya kijamii huku Hanscana pia akishiriki kumjibia Khalfan ambaye hufanya naye kazi pamoja.

“Mimi kiukweli ninawatakia kila lakheri, mimi sina kinyongo wala ubaya na wao nadhani waendelee, wakazane watu ndio wataamua,” alisema Nisher.

“Mimi kazi zao hazinitishi kwasababu catalogue yangu ndefu inaeleweka, issue tunayoangalia ni numbers. Ninaposema tunaangalia numbers tunaangalia vitu kama views, fan base, status, tunaangalia money – how much money are they making! Tunaangalia video yangu moja ni shilingi ngapi na video yako moja ni shilling ngapi, tuanze kuongea kuanzia hapo.”

“Ukishaweza kunifunika hapo nadhani tunaweza tukaongea sasa kwasababu tunakuwa equal. Lakini sidhani kama wanaweza wakajinadi kwamba wamefika, bado. Mimi mwenyewe bado sijafika nakazana, kuna mahali napataka sijapapata. So na wao wanapodhani kuwa wanakuwa wamenifikia wanakuwa wanakosea, lakini wakibaki na njaa kwamba tunataka tufike level kubwa watafika mbali.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents