Hapatoshi kombe la dunia ni Uruguay dhidi ya Ufaransa huku Brazil na Ubelgiji

Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuendelea hii leo kwa hatua ya robo fainali huko nchini Urusi baada ya kupita mapumziko ya siku mbili.

Leo siku ya Ijumaa timu nne zitashuka dimbani kuwakilisha nchi zao katika kuwani nafasi ya kutwaa kombe hilo wakati bingwa mtetezi Ujerumani akiwa tayari ameshafungashiwa virago mapema kwenye hatua za awali.

Mchezo wa kwanza utakuwa majira ya saa 11 jioni ambapo Uruguay itashuka dimbani kuikabili Ufaransa wakati saa 3 usiku timu ya taifa ya Brazil watakuwa na kibarua kizito mbele ya Ubelgiji.

Hapokesho timu ya taifa ya Sweden watakipiga  Uingereza wakati mwenyeji Urusi akishuka dimbani kuwakabili Croatia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW