Habari

Happy Birthday Hasheem Thabeet, hongera kwa kutimiza miaka 26 leo

5c7292cc457611e2b52122000a1fa4b5_7

February 16, 1987 jijini Dar es Salaam, Tanzania Hasheem Thabit Manka alizaliwa. Ndiye mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani.

Thabeet anayeichezea klabu ya Oklahama City Thunder (OCK) na ndiye mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi hiyo ya Marekani kwa sasa. Kabla ya kuingia katika rekodi hiyo, Hasheem mwenye umri wa miaka 26 aliyekulia mitaa ya Sinza, Dar es Salaam na ambaye hakuwahi kucheza mpira wa kikapu hadi anafikia umri wa miaka 15, alikuwamo katika orodha ya nyota 20 warefu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya NBA.

Hasheem 2

OKC ilimtwaa Thabeet akiwa mchezaji huru Julai mwaka jana, kwa makubaliano yanayotajwa kumhakikishia dola milioni 1.2 (Sh bilioni 2, sawa na Sh milioni 160 kwa wiki, achilia mbali malipo ya mikataba ya udhamini) katika msimu huu, kiasi kama hicho katika msimu ujao na dola milioni 1.25 katika msimu wa 2014/15.

Ingawa anatajwa kutong’ara sana katika misimu yake mitatu ya kwanza ndani ya NBA akiwa Memphis Grizzlies, Houston Rockets na Portland Trail Blazers, Meneja wa Thunder, Sam Presti alimtetea akisema Thabeet anaamini ataisaidia sana klabu yao kwani ana kipaji na pia umri unamruhusu kuendelea kujifunza.

d80ed25c448511e28d0622000a9e13b7_7
Kama ulivyo utabiri wa Presti, Thabeet ameanza kuitumikia klabu yake mpya kwa kishindo, ingawa alianza kwa kukabiliwa na majeraha.

1918c106165d11e28dc022000a1f8c21_7

Leo hii anatimiza miaka 26 kwa kutweet ujumbe mfupi: THANK GOD FOR ANOTHER YEAR OF HEALTHY MIND, BODY AND SPIRIT. #BDAY #TURNTFUP #BLESSED.

Happy Birthday Hasheem.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents