Happy Birthday: March 30, 1980 Godfather wa Bongo Flava, P-Funk alizaliwa

Japokuwa Bongo Flava ina historia ndefu, jina la P-Funk ni la muhimu zaidi kulipigia mstari. Majani aka Kinywele kimoja mwenye mchango usiosahaulika kwenye mafanikio ya Bongo Flava leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Majani1

Majani alizaliwa kwa jina la Paul Matthysse. Ana mchanganyiko wa kitanzania na kidachi. Kwenye Miaka 1991-92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika, Majani alikuwa mtundu kwenye studio za pale shule kwa kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka na pia alikuwa mbele kwa kupiga muziki kwenye party mbalimbali.

P-Funk alikwenda kimasomo ya (sound) engineering kwa miezi 18 mjini Amsterdam, Netherland kabla hajaingia kwenye kutayarisha muziki. Maisha ya huko hayakuwa rahisi kwakuwa alikumbana na ubaguzi wa rangi wa hatari.

Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi kilichorushwa December mwaka jana P alisimulia: Nilipokwenda kusoma Sound Engineering nilikaa na aunt yangu yeye anakaa kwenye kijiji ambacho hakuna waswahili, hakuna wahindi, wachina tu nao wachina wanapika Chinese tu pale basi. So ni kila siku asubuhi, alfajri inabidi nipande actually baiskeli niende kwenye train station nipande treni niende Amsterdam nirudi hivyo hivyo.

Sasa kuna siku moja nimeenda nimerudi nakuta vitoto hivi tunaviita skin heads, vinapenda kuvaa jacket jeusi halafu ndani ina orange nikaona wananiambia kwa kijerumani, ‘watu weusi toka nje ya nchi yetu, go away, ondoka’. Sasa mimi mtoto nilishadata nimetoka Masaki kule lakini nilikuwa nakaa na watu wa uswahilini, nilikuwa mtoto wa mama lakini si mtoto wa mama, mgumu! Mwanangu si nikawang’uta vizuri, pitisha mtu kwenye kioo cha Chinese pale, halafu kinachochekesha mmoja baba yake ndio mkuu wa polisi wa hicho kijiji.

Sasa ile story watu walivyoanza kuifuatilia, wale walikuwa sita. Nikakamatwa lakini akaja aunt yangu na ni mtu ana roho nzuri, aliweka sawa kisheria, and then from then on nikipita respect, ulaya ubaguzi ni mkubwa.

Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa.

Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo. Anakubali kuwa amepata sana utaalam na mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Majani ana orodha kubwa ya wasanii nchini aliowatoa wakiwemo Juma Nature, Jay MO, TID, Solo Thang, Ngwair, Fid Q, Zay B, Sister P, Rah P, Daz Baba, Ferooz, Man Dojo na Domo Kaya, Mike T na bila kusahau kazi nyingi za Profesa alizozifanya yeye.

Ni ukweli usiopingika kuwa, P Funk aka Khalfan ama Mkono wa Mungu ndiye producer wa Tanzania aliyetengeneza hits nyingi zaidi kuliko mwingine yeyote. Bongo5 inamtakia Happy Birthday producer huyu machachari. Bado ana mchango mkubwa tu kwenye maendeleo ya muziki wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents