Habari

Happy birthday to our very own Miss Africa, the beautiful Nancy Sumari

Leo tumesherekea kwa kuzaliwa kwake Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari, mshiriki pekee kutoka Tanzania katika mashindano ya Miss World ambaye alifanikiwa kufika hatua za mwisho na kunyakulia taji la Miss World Africa.

Mabalozi wa TEA Faraja Kota na Nancy Sumari wakimchangisha Mh. Cheyo

Yeye binfasi aliamua kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwa style tofauti, akiongozana na mabalozi wenzake wa kampeni ya ‘Elimu yao Wajibu Wetu’ Faraja Nyalandu na Rebeca Gyumi walifika bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.

Mabalozi wa Changia Tofali, Nancy Sumari, Rebeca Gyumi na Faraja Nyalandu wakipozi na Naibu Waziri January Makamba

Msomaji wetu ukitaka unaweza kuchangia pia kwa kutuma ujumbe fupi wa SMS yenye maandishi CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564, na utatozwa Tsh 250. Lengo la kampeni ni kuchangia ujenzi wa hostel 30 ambazo zitawahudumia wanafunzi wa kike 1,504.

Mabalozi wa TEA walipotembelea sekondari ya Kibaigwa

Mungu awabariki kwa jitihada zenu, wadau tukumbuke kwamba jukumu la kujenga taifa letu ni la kwetu sote! Je wewe umchangia?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents