Burudani

Harmonize aachwa solemba na mapromota uchwara nchini Kenya, awaomba radhi mashabiki wake

Msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania, Harmonize amejikuta akishindwa kupanda jukwaani kutumbuiza mjini Eldoret nchini Kenya baada ya Promota aliyemleta kushindwa kumalizia mkwanja wake kama walivyopatana.

Harmonize

Harmonize akielezea sakata hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kuwa Promota huyo alipotea dakika za mwisho jambo ambalo lilizua taharuki kwa watu ambao walikuwa wameshalipia kiingilio kumtazama.

BINAFSI NAJUA KIASI GANI PESA INATAFUTWA KWA UGUMU BUT KWA MAPENZI YENU MLIJITOA KUJA KUNI SUPPORT SIO KWASABABU MIE NI SPECIAL SANA….!!! NI KWA UPENDO WENU TUU ILA KILICHONISIKITISHA NI PROMOTERS KUCHUKUA PESA ZA WATU WASIO PUNGUA 4000K THEN WAKASHINDWA KUJA KUMALIZIA PAYMENT ILIYOBAKI NA KUKIMBIA HII INAUMIZA SANA…!! (1) NI DALILI YA KUNIVUNJIA HESHIMA NA UAMINIFU KWA MASHABIKI ZANGU (2) IMENIUMIZA KUONA WATU WALIOJITOA KULIPA VIINGILIO VYAO JUST FOR ME WANADHULUMIWA MWISHO KABISA…!!! NISEME SAMAHANI #ELDORET 🙏🙏 NEXT TIME NITAHAKIKISHA TUMELIPWA DOO YOTE KABLA NI COME TRUST ME I’M SO….!!! DISAPPOINTED AND I LOVE YOU ❤ AND I WAS EXTRA READY 👹👹 I DID#SOUNDCHECK AND EVERYTHING THIS IS TO BAD

Harmonize usiku wa kuamkia leo alitakiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo la muziki mjini Eldoret kabla ya kuzinguliwa na promota huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents