Burudani

Harmonize aanza kuweka wazi video ya ‘Kwa Ngwaru’

By  | 

Wakati mashabiki wakisubiri kwa hamu kubwa video ya ngoma ya ‘Kwa Ngwaru’ ya Harmonize ambayo amemshirikisha Diamond, tayari picha za video hizo zimeanza kusambaa.

Harmo kupitia mtandao wake wa Instagram ameweka picha hiyo ambayo inawaonyesha wakati walipokuwa wanashoot video hiyo ambapo kuna uwezekano mkubwa ndio picha ya video ya wimbo huo.

Kutokana na ujio wa picha hizo tutarajie kuona video ya wimbo huo ikitoka muda sio mrefu.

Wakati huo huo audio ya wimbo huo tayari imesikilizwa zaidi ya mara milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments