BurudaniUncategorized

Harmonize akiri kusikiliza nyimbo za Alikiba

Msanii wa Bongo Flava, Harmonize amesema anapenda kusikiliza nyimbo za wasanii mbali mbali akiwemo Alikiba.

Muimbaji huyo anafanya kazi chini ya label ya WCB ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz ambaye imekuwa ikivumishwa kutoelewana na Alikiba.

“Zamani sana zilikua nasikiliza nyimbo za Ali, nafikiri ilikuwa Mac Muga  kama sikosei, Mac Muga nilikuwa nasikiliza sana, so… hivyo!,” amesema Harmonize katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm.

Awali alitangulia kusema kuwa huwa anapenda kusikiliza ngoma za wasanii wengi sana hususani wa Tanzania kwa sababu anaamini akiwasikiliza wasanii wenzake anajifunza vitu vingi.

“Siyo Ali pekee yake kuna nyimbo za wasanii wengi nasikilizaga, namsikilizaga Barnaba na wasanii wengine waimbaji wa WCB na nje ya WCB pia,” amesema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents