Burudani

Harmonize atoa baraka zote kwa Zari kumbwaga Diamond

Stori za ua jeusi la aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady bado zipo kwenye headlines, hatimaye Harmonize amezungumzia hatua ya Zari kuachana na Diamond.

Muimbaji huyo wa WCB ameiambia Funiko, Radio Five kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa kuwa ana sababu zake za msingi.

“Mimi na heshimu sana maamuzi ya mtu, siwezi kuzungumza kama ni vibaya au ni vizuri, kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu mahusiano ndio sina,” amesema.

Alipoulizwa iwapo kipindi wawili hao walikuwa katika mahusiano kuna baadhi ya vitu alinufaika navyo kutoka kwa Zari, Harmonize alijibu;

“Kuzungumza amenisaidia au hajanisaidi sio kitu kizuri halafu kwa njia moja au nyingine unaweza kuonekana ni mnafiki, kwanini usiseme siku zote uje useme leo,” alieleza.

Soma Pia; Mahusiano ya Diamond na Zari bye bye

Mnano February 14 mwaka huu katika siku ya wapenda nao Zari The Boss Lady ambaye ni mzazi mwenzie na  Diamond Platnumz, aliposti Ua Jeusi katika mtandao wa Instagram na kutangaza kuachana kimahusiano na msanii huyo rasmi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents