Tia Kitu. Pata Vituuz!

Harmonize atoa msaada kwa walemavu ” Sijakamilika hasa ukichanganya na ujana” (+ Video)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB iliyochini ya Diamond Platnumz, Harmonize alimaarufu Kondeboy ameamua kutoa msaada kwa walemavu jijini Dar Es Salaam maeneo ya Kariakoo.

Msanii huyo ameamua kurudisha shukrani hizo kwa mashabiki zake ambao wana matatizo mbalimbali hasa walemavu wa miguu na katika kipindi hiki ambapo tumeingia mwaka mwingine.

Mbali na kutoa msaada huo msanii huyo ameandika ujumbe mrefu sana kweny ukurasa wake wa Instagram akitoa shukrani zake kwa wale wote walioweza kwa namna moja ama nyingine kuusapot muziki wake. na Ukumbe mwenyewe ndio huu hapa:-

“HERI YA MWAKA MPYA….!!! NDUGU ZANGU …!!! NINGEPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WAANDISHI WA HABARI PAMOJA NA MEDIA ZOTE AMBAZO ZIMEKUWA SAMBAMBA NAMI BILA KUWASAHAU DJ’S WOTE DUNIANI KWA KUUNGANA NAMI NA KUNI SUPPORT KUSOPPORT MUZIKI WANGU AMA KWA HAKIKA BILA NYINYI BASI PASINGEKUWA NA HARMONIZE HATA MUZIKI WENYEWE HUWENDA USINGEKUWEPO MWAKA 2018 UMEKUWA MWAKA WENYE KUONYESHA MWANGA AMA NURU YA MUZIKI KWANGU NAAMINI MAZURI MENGI YAPO MBELE NINGEOMBA MUENDELEE NA MOYO HUWO HUWO WA UPENDO NA IMANI KUNIVUMILIA NINAPOKOSEA KWANI MIMI SIJAKAMILIKA HASA UKICHANGANYA NA UJANA…!!!! LAKINI PIA NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA SHABIKI ZANGU AMBAO MUPO BEGA KWA BEGA NAMI KUHAKIKISHA TUNALIKAMILISHA KILA TULIPANGALO KWA UWEZO WA MUNGU….!!!!! HAKIKA NYINYI NDIO HARMONIZE MWENYEWE….!!! LAMWISHO NIOMBE KUWASILISHA HILI DOGO KWA WAMILIKI WA MEDIA WATANGAZAJI PAMOJA NA DJ’S WOTE….!!! KAMA UNGEPENDA MIMI NIKUPIGIE JINGLE AU TANGAZO LA REDIO YAKO BASI UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUCHUKUA NUMBER HI..! 👉 +255658135762 KISHA TUMA MAELEKEZO YAKO MFANO MIMI NI DJ FULANI KIPINDI FULANI YANI TUMA MAELEKEZO YAKO YOTE KUPITIA WHTSP NADHANI WATU WA MEDIA WASHANIELEWA NINACHO MAANISHA KISHA MWISHO WEKA EMAIL YAKO NAMI NITARECORD NA NITAKUTUMI KATIKA EMAIL YAKO HI NI KWA MEDIA WATANGAZAJI DJ’S WOTE DUNIANI……!!! LET’S GO…….!!!!!!!!!!”

Msanii huyo amekuwa sio mara ya kwanza kwenda kutoa msaada Kariakoo sehemu ambayo inaaminika ndio yalikuwa makzi ya msanii huyo kwani alishawahi kufanya kazi hapo ya kuuza maji kabla ya kuwa msanii.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW