Burudani

Harmonize awatambia Diamond na Rayvanny kuhusu Wasafi Festival kufanyika Mtwara, Diamond amjibu

Harmonize awatambia Diamond na Rayvanny kuhusu Wasafi Festival kufanyika Mtwara, Diamond amjibu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize ‘Konde boy’ jinsi anavyojiita kwa sasa,amefunguka mwanzo mwisho na kutoa hisia zake kuhusu Tamasha la Wasafi ambalo linatarajiwa kuanza mwezi huu wa 11 tarehe 24 mjini Mtwara.

Harmonize ameongea hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuongea hayo baada ya tamasha hilo kuzinduliwa jana katika ofisi za Wasafi jijini Dar Es Salaam.

Katika uzinduzi huo Harmonize hakuwepo kwani yuko Kenya kwa ajili ya tour yake. na wakati wa uzinduzi Diamond aliongea kuhusu tamasha hilo ambalo litaanzia Mtwara akimtania Harmonize, ” Najua Wanamtwara watamsapoti sana Harmonize kwa sababu anatoka huko ila mimi nimejipanga sana na kama unavyojua sisi wasanii wa WCB tunapenda kukamiana na kuahidi atafanya show kali sana hata kama Harmonize anatokea Mtwara”

Baada ya hayo Harmonize aliposti video inayoonyesha slogani yao ambayo ni “Huu mchezo usiuchezee wewe kabisaaa” na Harmonize kusema ” MTWARA….!!!! NADHANI MNAONA MWANENU NINAVOWAPAMBANIA…!!! YANI HAIJAANZA #KIGOMA KWAKINA @diamondplatnumz WALA MBEYA KWAKINA @rayvanny INAANZIA MTWARA……!!!!! MIKONO JUU…..!!!! 🙌🙌🙌🙌🙌🙌 #MCHEZOUSIUCHEZEEWEWEEEKABISAAAAAA……!!!!

lakini baada ya kuandika hivyo Diamond nae akamjibu hivi akianza kwa kucheka ”  Hahahahahh Unatamba mdogo wangu…….! Sawa bana”

Harmonize alirudi tena akianza kwa kumtag Diamond na kusema “Hii inaenda kuwa asante na kwa heri……!!!! Asante kwa kunikubalia ombi langu.”

Ikumbukwe Wasafi media wametangaza mikoa mitano ya awali ambayo watakwenda kutumbuiza katika tamasha hilo ambayo ni Mtwara, Iringa, Morogoro, Zanzibar na Dar Es salaam, mbali na mikoa hiyo pia tamasha hilo litafanyika hadi nje ya nchini ambapo litafika nchini Kenya katika maeneo mawili ambayo ni Nairobi na Mombasa.

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents