Burudani

Harmonize: Sijui kama Diamond aliwahi kuwa na uhusiano na Wolper

Harmonize ameendelea kusisitiza msimamo wake kuwa hajawahi kusikia kama Diamond na mpenzi wake Jacqueline Wolper waliwahi kuwa na mahusiano.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, muimbaji huyo amekana kabisa kuwahi kusikia kama mpenzi wake huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bosi wake ambaye ni hitmaker wa Marry You.

“I don’t know about that, sijui kama Jackie alishawahi kudate na Chibu D. Sijui na sijawahi kusikia. Mimi mwanakijiji bro mjini sijafika siku nyingi, so sijui na sijawahi kusikia ndio kwanza unanisuprise. Kumbe ilishawahi kutokea hivyo?,” amesema Harmo.

“Confirmation niliyokuwa naihitaji sio hiyo bro, nilikuwa nataka confirmation kutoka kwa Diamond kwamba anaonaje mimi nikikaa pale kwa Wolper. Alinijibu kuwa ni mwanamke mzuri lakini hakuniambia kama alishawahi kudate naye na wala Jackie hajawahi kuniambia kama alishawahi kudate na Diamond,” ameongeza.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Niambie’ ambapo video yake imeshatazamwa mara 571k katika mtandao wa Youtube japo ina siku tano tu tangu ilipotoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents