Michezo

Harry Kane atinga orodha ya wafungaji hatari Uingereza

By  | 

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane ameingia katika orodha ya wachezaji ambao wamefunga magoli 100 na kuendelea katika ligi kuu ya Uingereza.

Kane ambaye jana (Jumapili) alifunga bao moja katika mchezo ambao Spurs ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Liverpool, ameingia katika orodha hiyo baada ya kufikisha magoli 100 kati ya mechi 141 aliyochezea timu hiyo.

Katika orodha hiyo Kane anashika nafasi ya 26, wakati nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Alan Shearer, ambaye alifunga magoli 260 katika ligi hiyo kabla haja staafu.

Katika magoli hayo 100 aliyofunga Kane, mabao 26 amefunga kwa mguu wa kushoto na mengine 60 amefunga kwa mguu wake wa kulia. Wakati huo huo mabao mengine 14 amefunga kwa kichwa.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments