Burudani

Harusi ya Kanye West na Kim Kardashian kurushwa kama kipindi maalum chenye part 1 & 2 kupitia E!

Harusi ya rapper Kanye West na Kim Kardashian ndio gumzo kubwa kwa sasa mitandaoni, wakati wengi wakiwa wanaisubiri kwa hamu kituo cha runinga E! kimeanza maandalizi ya kurusha tukio hilo.

Kanye+West+Kim+Kardashian+Gets+Engaged+Kanye+myMXjckbpBrl

Imethibitishwa kuwa harusi ya mwaka ya mastaa hao itaoneshwa kupitia kituo cha runinga E! kama kipindi maalum katika sehemu mbili (Part 1 & 2).

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, tukio hilo kubwa kwa wawili hao halitakuwa sehemu ya reality show ya familia ya Kardashian KUWTK (Keeping Up With The Kardashians) kama ilivyodhaniwa na wengi, kwasababu wao tu wawili ni wakubwa sana na wana uwezo wa kuwa na show yao wenyewe maalum. Chanzo kimoja kiliuambia mtandao wa Hollywoodlife.

“They have filmed some things already to be on the upcoming special and will film stuff afterwards as well. But the Kim and Kanye special will be a stand-alone show on E!,”

Nyota hao wanatarajiwa ku-tie the knot (May 24), huku harusi yao ikitarajiwa kuwa moja ya harusi kubwa kuwahi kufungwa za mastaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents