Michezo

Hasheem kufungua Clinic

 

Mchezaji wa Mpira wa kikapu nchini Marekani NBA anayechezea timu ya Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet aalitangaza ndani ya kipindi cha Jahazi kupitia redio ya Clouds FM kuhusiana na kuanza kwa programu ya Basketball Clinic itakayoanza Agosti 12 kwenye viwanja vya Don Bosco jijini.

Zaidi ya watu 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo ambapo TBF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Phares Magesa amesema wanatakiwa kujiandikisha katika shule zote zenye vilabu vya Basketball nchini kote.

Lakini pia Hasheem Thabeet ameeleza kwamba katika nchi za Afrika ameshafanya Basketball Clinic kama hizo katika nchi za Nigeria, Senegal, Ivory Coast pamoja na Tanzania kwa sasa, kwa nchi za Asia amefanya programu kama hiyo na mchezaji mwenzake Yao Ming kwa nchi za HongKong, Quatar na Taipei, kulia katika picha ni mtangazaji wa kipindi hicho Capt. Gadna G Habash na mwsiho kati Ephrahim Kibonde.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents