Burudani

Hasheem Thabeet ampigia saluti Wakazi, azitaja nchi mbili za Afrika ambazo muziki wake unapigwa zaidi Japan (+video)

Mchezaji wa kikapu Mtanzania, Hasheem Thabeet ambaye kwa sasa anakipiga kunako timu ya Yokohama B-Corsairs ya nchini Japan amefunguka jinsi msanii wa muziki wa hip hop, Wakazi alivyomsaidia kumtambulisha kwa Watanzania wanaoishi nchini Marekani kipindi hicho wakati anacheza Ligi ya NBA.

Hasheem pia ameeleza maisha yake ya sasa nchini Japan ambapo ameelezea ishu za ubaguzi wa rangi kwa kudai kuwa vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini hajaviona kabisa.

Kwa upande mwingine Thabeet ameitaja nchi za Kenya na Nigeria kuwa ndio nchi za Afrika ambazo muziki wao unapigwa zaidi kwenye sehemu za starehe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents