DStv Inogilee!

Hasheem Thabeet atikisa vichwa vya habari barani Ulaya, kurejea NBA muda wowote

Mchezaji wa kikapu maarufu kama Basketball nchini Tanzania, Hasheem Thabeet amegonga vichwa vya habari barani Ulaya baada ya kuhusishwa kurejea kwake kwenye ligi ya mchezo huo NBA huko Marekani.

Mara baada ya kumalizika kwa michezo ya ‘All-Star weekend’ Jumapili iliyopita ndipo kukaibuka taarifa za kurejea kwa mwanakikapu huyo pandikizi la mtu mwenye urefu wa futi saba (7) na nchi tatu (3). kwenye ligi ya NBA.

Wakati zimesalia wiki mbili na nusu kabla ya kufungwa kwa dirisha la biashara za wachezaji, taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya zinasema kuwa mpaka sasa klabu tatu zimejitokeza kusaka saini yake ambavyo ni Houston Rockets, Toronto Raptors pamoja na Detroit Pistons.

Inaaelezwa kuwa Mkurugenzi wa Houston Rockets, Daryl Morey anahitaji kumsajili nyota huyo wa Tanzania ili kuboresha timu yake, huku akihitaji kukwepa gharama kubwa ya usajili msimu huu.

Thabeet, amewahi kuitumikia timu ya Oklahoma City Thunder (OKC) inayoshiriki ligi ya NBA akisajiliwa kama mchezaji huru mwaka 2012.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, mara ya mwisho kucheza ligi pendwa ya Basketball nchini Marekani NBA ilikuwa ni mwaka 2013-14.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW