Michezo

Hasheem Thabeet kushuka dimbani kwa mara ya kwanza wiki hii

Mtanzania, Hasheem Thabeet ambaye amesajiliwa na klabu ya Yokohama B inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Japan ‘B1 League’ anatarajia kuanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya timu ya Levanga Hokkaido katika dimba la kimataifa la Yokohama ‘Yokohama International Arena Pool’.

 

Thabeet atacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Levanga Hokkaido Oktoba 7 ya wiki hii ikiwa ni tangu alipojiunga na timu hiyo Septemba 28 mwaka huu.

Hasheem Thabeet aikacha NBA atimkia Japan

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji wazamani wa klabu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’, amecheza jumla ya michezo 224 NBA ikiwa ni sawa na wastani wa pointi 2.1 na mitupo 2.6 ‘rebounds.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents