BurudaniMitindo

Hassanali na TWENDE

 

Kwa mara ya kwanza mbunifu maarufu wa mavazi Tanzania Mustafa Hassanali (pichani) ameandaa onesho kwa wajasiriamali wanawake, onesho hilo litajulikana kwa jina la TWENDE (Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development Exposition).

Onesho hilo litafanyika kwa muda wasiku mbili, tarehe 16 na 17 mwezi wa Septemba 2010, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, na kuwashirikisha wajasirimali wanawake zaidi ya 100 kutoka pembe zote za nchi, wafanya biashara kutoka viwanda vikubwa na vidogo,taasisi za serikalini na mashirika yasio ya kiserikali yaani NGOs.

“TWENDE imepanga kuleta maendeleo ya wanawake kwa kuandaa tukio ambalo litawakutanisha pamoja wanawake wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwaniili waweze kuonesha kazi zao, kujitangaza na kuuza bidhaa zao. Sambamba na semina ya siku mbili itakayotoa elimu bora juu ya maswala ya kibiashara kwa wajasiriamali watakaoshiriki”, Alifafanua Mustafa.

Lengo kuu la kuandaa TWENDE ni kuendeleza na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa kwa kutambua uwezo wao na mafanikio ya wajasiriamali wanawake, ukijumisha na wale wenye ulemavu ili kuleta ajira na maendeleo kwa wote.

Pia ni kuonesha wajasiriamali wanawake kama mfano wa kuigwa, kuongeza juhudi za maendeleo ya wanawake wajasiriamali, kutoa ujumbe na kubadilishana mbinu mbalimbali za kibiashara, kuwajenga wafanyabiashara wanawake na kuazisha SACCOS (TWENDE SACCOS), kuendeleza uzalendo wa kutumia bidhaa za watanzani, sambamba na kutengeneza jukwaa kwa ajili wa wanawake wenye uwezo mdogo, kati, mkubwa na wale kutoka kwenye taasisi zisizokuwa za kiserikali kukaa pamoja na kupanga mikakati itakayowezesha kufanikiwa zaidi, na kutengeneza mahusiano ya wanawake wajasiriamali kimkoa, kitaifa na kimataifa.

Ujumbe wa maonesho ya TWENDE, “Mimi ni mwanamke, mimi ni mjasiriamali, nikiwezeshwa ninaweza, mwanamke maendeleo”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents