Michezo

‘Hat-Trick’ kumpa ugali Philippe Coutinho, Bayern Munich

Mastaa wa Bayern Munich wameuwomba uongozi wa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Bundesliga kumpatia mkataba wa kudumu mchezaji mwenzao, Philippe Coutinho baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mchezo wao dhidi ya Werder Bremen na kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 6-1 uliyopigwa Jumamosi hii.

Philippe Coutinho's Bayern Munich team-mates are desperate for him to be signed outright

Nyota huyo wazamani wa Liverpool, alikuwa moto wa kuotea mbali siku hiyo ambapo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu ‘hat-trick’ peke yake kati ya sita (6) waliyoshinda dhidi ya Werder Bremen, hali iliyopelekea wachezaji wenzake kuomba apewe kandarasi ya kudumu.

Coutinho yupo hapo kwa mkopo akitokea Barcelona na tayari ameshajijengea mashabiki wengi nchini Ujerumani. Na kwa sasa wachezaji wenzake wanajaribu kumuombea ili aweze kubaki hapo moja kwa moja.

The on-loan Barcelona man fired in a sensational hat-trick in Bayerns 6-1 demolition of Bremen

”Ilikuwa kitu bora sana alichofanya hii leo, tunahitaji aina hii ya mchezaji, hakika nimefurahi sana ameonyesha kile anachoweza kufanya,” amesema Robert Lewandowski

David Alaba pia kwa upande wake amesema kuwa ”Kama umeweza kutizama mchezo wa leo, basi tunapaswa tumnunue, si ndiyo ?.”

Coutinho's hat-trick included a classy chip and trademark curling effort into the far corner

Hata hivyo ili uweze kumnunua Mbrazil huyo basi lazima ujiandae na kitita cha pauni milioni 100 kutokana na mkataba wake, na Bayern tayari iliamua kuwekeza fedha zake kwa kinda wa miaka 20 wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents