Burudani

‘Hata wana hip hop tuna hisia’ – Stamina

Rapa kutoka Morogoro, Stamina amefunguka na kusema kuwa ameamua kuimba wimbo wa mapenzi, siyo kwa sababu nyimbo zake ngumu zimebuma bali amebadilika kidogo ili kuimba vitu vilivyopo kwenye jamii kwa kuwa yeye ni msanii pia kama wengine.

Stamina akiwa na Maua Sama wakati wa utengenezaji wa video ya wimbo wake mpya wa ‘Love me’

Stamina anaefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Love Me’ aliomshirikisha Maua Sama amesema kwamba ujio wake mpya ameamua kuimba maisha yaliyopo kwenye jamii inayomzunguka na kuongeza kuwa hajatoa kwa sababu ameumizwa kimapenzi bali yeye kama msanii ni wajibu wake kwa kuwa mapenzi ni maisha yaliyopo kwenye sehemu ya jamii.

“Naamini hakuna kitu kigumu mbele ya mapenzi kwani hata wana hip hop tuna hisia kama watu wengine, Sijatoa ‘Love me’ kwa sababu nimetendwa ila nimeimba kuwasilisha kazi ya sanaa kwa sababu mimi ni msanii, Mwana hip hop akitoa nyimbo ya mapenzi watu wanamshangaa kwani sisi ndio hatuna wapenzi? mapenzi ni sehemu ya maisha”,alisema stamina kwenye mahojiano yake na EATV.

Hata hivyo Stamina alisisitiza kuwa hakuna sababu yoyote iliyomsukuma kuimba mapenzi hii ni baada ya watu kuzungumza mitandaoni kuwa ameamua abadilishe muziki wake ili auze zaidi na kupiga show.Unaweza ukatazama wimbo huo mpya wa Stamina na Maua Sama hapa chini

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents