Burudani ya Michezo Live

Hati yatolewa viongozi wanne wa CHADEMA wakamatwe, Yupo Halima Mdee na Ester Bulaya

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu leo Novemba 15, 2019 imetoa hati ya kukamatwa kwa viongozi wanne wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Ester Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche kwa kutohudhuria mahakamani hapo bila taarifa yoyote katika kesi yao Uchochezi inayowakabiri.

Mahakama hiyo pia imetoa hati ya wito kwa wadhamini wa washtakiwa hao, Wafike mahakamani hapo kujieleza kwanini hawakuwapeleka washtakiwa mahakamani kama masharti ya dhamana yanavyowataka.

Washtakiwa waliofanikiwa kufika mahakamani hapo leo ni  Mwenyekiti wa CHADEMA,  Freeman Mbowe,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.

Viongozi hao wa CHADEMA wanakabiliwa na  mashtaka 13, Ikiwemo uchochezi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19, 20 na 21, mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW