Burudani

Hatima ya Nedy Music PKP baada ya Ommy Dimpoz kusaini RockStar4000

Mmiliki wa label ya PKP, msanii Ommy Dimpoz baada ya kusaini RockStar4000 ameeleza hatima ya Nedy Music ndani ya PKP.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Cheche’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa Nedy Music atakuwa na timu yake ya kumsimamia lakini PKP ipo pale pale.

“Ni vitu muhimu sana msanii kuwa na menejimenti, hata Nedy nimemtengenezea timu ambayo itakuwa inamsimamia mambo yake, kwa hiyo mimi sina he deck hivyo tunasimamia biashara yetu ya PKP kwa sababu tumewekeza pale, hakuna kilichoharibika, Kanye West alikuwa chini ya Jay Z lakini ana Good Music,” amesema Ommy Dimpoz.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents