Michezo

Hatima ya Stars na Wapalestina leo

palestine

 

Timu ya Palestine inayoundwa na baadhi ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika nchi mbalimbali barani Asia na Ulaya, kwa mara ya kwanza watacheza soka Barani Afrika na timu ya Taifa Stars leo.

Akizungumzia hatua hiyo, Balozi wa Palestine nchini, Navi Abu Jeish alisema suala la Tanzania kukubali kucheza na Palestine mechi ya kirafiki ni heshima kubwa ambayo itaendeleza kudumisha uhusiano muzuri wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Alisema timu yao imekuwa ikishindwa kucheza mechi mmbalimbali za kirafiki kutokana na hali mbaya ya kisiasa iliyopo kati yao na Israel jambo ambalo limesababisha kuwa chini zaidi katika viwango vya soka vya  Duniani.

“Tunaishukuru Tanzania kwa kutukubalia kucheza nao hivyo hali hii ni moja ya heshima kubwa kwetu ambayo kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuimarisha historia nzuri iliyopo kati yetu na wananchi wa Tanzania.

“Kwa hakika tumekuwa tukipata wakati mugumu sana kupata mechi za kirafiki, hii ni kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwetu hivyo kupata mechi hii ni moja ya mafanikio makubwa na tunaishukuru Tanzania kwa hilo,” alisema Jeish.

Katika hatua nyingine Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewasihi Watanzania kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars na kutambua kuwa mechi hii ya leo in muhimu sana kwa timu hiyo.

Alisema kutokana kutambua mchango wa wapenzi wa soka nchini viingilio vya mechi hiyo vitakuwa vya chini na ambavyo vitamwezesha kila momja kuangalia mchezo huo ambao utaandika historia mpya ya soka Tanzania na Duniani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents