Habari

Hatimaye aliyepasuliwa kichwa kwa makosa apelekwa India

MUATHIRIKA wa upasuaji tata uliofanyika katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Emmanuel Didas jana alisafirishwa kwenda India kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Andrew Msechu na Jacson Odoyo


MUATHIRIKA wa upasuaji tata uliofanyika katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Emmanuel Didas jana alisafirishwa kwenda India kwa uchunguzi na matibabu zaidi.


Didas ambaye awali alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu baada ya kupata ajali ya pikipiki badala yake akafanyiwa upasuaji wa kichwa, anapelekwa katika Hospitali ya Indra Prastha Apollo ya New Delhi, ambapo atafanyiwa uchunguzi na kisha kupata mkatibabu kulingana na maelekezo ya madaktari bingwa nchini humo.


Didas ambaye tangu kufanyiwa upasuaji huo Novemba Mosi, ingawa ana nafuu, hali yake bado haijarejea kama awali na jana alionekana kuweza kutambua baadhi ya mambo, pia kuzungumza kwa taabu.


Mara alipokuwa akitolewa kwenye wodi na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa la Kitengo cha Tiba na Dharura cha Kampuni ya Ultimate Security yenye namba T 974 AQW saa 6.00 mchana, Didas alionekana kuushangaa umati wa wauguzi waliokuwa wakimsindikiza pamoja na wanahabari waliokuwepo hospitalini hapo.


KIjana huyo aliweza kuinua kichwa chake na kutoa ishara ya kupunga mkono kwa taabu, kutokana na mwili wake kutokuwa na nguvu, lakini pia kuzungumza maneno machache yasiyoeleweka.


Hata hivyo, baada ya kufika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, aliweza kuzungumza maneno machache, akilalamikia uchovu na maumivu kwenye mgongo wake.


Hakuwa mwepesi kuzungumza wala kutoa majibu ya baadhi ya maswali aliyoulizwa japokuwa alionekana kutaka kujibu na kuzungumza na watu wengine.


Didas aliyesindikizwa na Muuguzi Germana Gasper kwenda India, aliondoka jana saa 9:00 alasiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (5yKQd) kuelekea nchini India kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Pia aliongozana na kaka yake, Sists Marishay.


Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Mubimbili, Almasi Jumaa aliyeongozana nao hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, alisema kuwa mgonjwa huyo �Ana tatizo lake la awali (la mguu), na hili jingine alilopata baada ya kufanyiwa upasuaji, lakini hasa anatakiwa kuchunguzi na baadaye kupatiwa matibabu kutokana na uchunguzi�.


Alisema matatizo yanayotakiwa kufanyiwa uchunguzi ni uwezekano wa kumaliza tatizo alilonalo baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa na uwezekano wa kushughulikia tatizo lake la awali, ambalo ni uvimbe kwenye.


Awali, pamoja na matatizo mengine, Didas aliripotiwa kupooza upande wa kulia wa mwili wake, alionekana kuwa na nguvu zaidi na kutumia mkono wake wa kushoto ambao alikuwa na uwezo wa kuugeuza atakavyo, tofauti na ule wa kulia ambao bado ulikuwa ukilazimika kuinuka kwa msaada.


Kufuatia hali hiyo, iliilazimu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kufanya maandalizi kwa ajili ya kumpatia matibabu zaidi nchini India, safari iliyoanza jana.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents